Saturday, October 09, 2010

NITASIMAMISHA MASOMO AU LA?

Ndugu wasomaji, ni wiki moja tu baada ya wizara ya elimu nchini Rwanda kuamua kwamba kuanzia januari mwaka wa 2011, haitaongeza kuasaidia wanafunzi wanaosomea vyuoni nchini humo kwa kuondoa elfu 25 za rwanda walizokuwa wakipokea kutoka kwa serikali ili ziwasaidie.
"Serikali ya Rwanda imeamua kwamba itasimamisha fedha elfu 25 zilizokuwa zikipewa wanafunzi kila mwezi kuanzia mwaka elfu mbili na kumi na moja". hayo ni maneno ya waziri wa elimu Bw. Charles MULIGANDE.Ameongeza kwamba fedha hizo zitawekwa katika shughuli nyingine zinazohusika na uboreshaji wa elimu nchini ikiwemo ununuzi wa mashine za kitekinelojia na vitabu.
Asilimia kubwa ya raia wa Rwanda ikiwemo wanafunzi huishi katika umaskini,na inajulikana kwamba fedha zile zilikuwa zikiwawezwsha wanafunzi kupata chakula, sabuni na kulipa kodi za nyumba ili waweze kuendelea na masomo.
Je, wanafunzi hawa watasimamisha masomo au la?
 Nimejaribu kuzungumza na baadhi yao, idadi kubwa ikasema kwamba huyu ni wakati wao wa kusimamisha masomo na wengine wakasema watafanya liwezekanalo ili wamalize masomo yao.
Lakini, kwa upande wangu najiuliza huyu kwli ni wakati mwafaka kwa serikali kuchukua uamuzi huwo?
Wanyarwanda tumepita katika mazuli na mabaya sote tunajua kwamba umaskini ni miongoni mwa athari kubwa zinazokumba nchi yetu, kuchukuwa uamuzi huwo ni kama kusahau kwamba asilimia kubwa ya wanyarwanda hawana uwezo wa kutosha ili wajisimamie wao wenyewe ndiyo sababu wanafunzi hawa wanahitaji kusaidiwa.
Ndugu wasomaji mlango mmoja ukifungwa mwingine hufunguliwa,Mungu ndiye muumba na atafanya ajabu kwa hali hiyo ,msiogope.Hamkumbuki yaliyowafikia wenzenu wa kidato cha kwanza, wakati walipoambiwa kwamba serikali haina uwezo wa kulipa fedha za shule? Basi mola hakutenda? Na kwa imani yangu na yako nadhani kupitia raisi tuliyechaguwa kwa asilimia kubwa akishilikiana na wabunge hawatalikubali hilo.
Vijana msiogope ni wakati  mzuri wakumuabudu Mungu.
Kwa upande mwingine ni wakati wa kujifunza kufanya kazi ili mjisaidie niyi wenyewe . Wanyarwanda wenzangu, katika karne zijazo zitakuwa ni zakujitegemea bila kungoja misaada ya kifedha lakini serikali nawambia pole pole ndiyo mwendo na simba mwenye kimya ndiye mla nyama na kwa wanafunzi akufundishaye kumtega samaki ataka upate wengi. Ewe serikali sikiliza vilio vya wanafunzi hawo na sasa macho yawo yanakuangalia, ikumbukwe kwamba kidole kimojahakivunji chawa  wanahitaji misaada yenu. Ahsanteni. 

No comments:

Post a Comment