Wednesday, September 22, 2010

Afrika inasema inaweza kufanya zaidi katika malengo ya Milenia


New York:
Viongozi wa Kiafrika wamesema wanaweza kufanya mengi zaidi ili kuyafikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza umaskini na kupambana na magonjwa na njaa. Akizungumza katika mkutano wa  kilele wa Umoja wa Mataifa mjini New York wa kutathmini kilichofikiwa katika kutekelezwa malengo ya Milenia, Rais wa Liberia, Ellen Johnson-Sirleaf, alisema ana imani Afrika inaweza kukabiliana na mitihani hiyo
Hapo kabla, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani alizitaka nchi zinazoendelea sio maisha zitegemee misaada. Alisema lazima nchi hizo ziongoze zenyewe mustakbali wao, na kuhakikisha kwamba rasilmali zao zinatumiwa kwa njia ilio sawa. Maendeleo ya kufikia malengo ya Milenia yamekwama kutokana na mzozo wa fedha duniani, na inakisiwa kwamba si chini ya dola za Kimarekani bilioni 120 bado zinahitajiwa kuyafikia malengo hayo, ambayo ni pamoja na kuupunguza umaskini kwa nusu.


No comments:

Post a Comment