Tuesday, August 24, 2010

Methali zinazoeza kukusaidia

.>Adabu ni dhahabu matendo ya heshima, staha na tabia njema ni Adabu.dhahabu ni kito cha thamana.Kitu chenye thamani kubwa.kwa maelezo mengine ya methali hii, mtu angeweza kusema kuwa ; kuwa na adabu ni kuwa na kito chenye thamani kubwa sana. ni utajili mkubwa katika maisha ya mtu kuliko utajili wa mali.methali hii ni funzo kwamba utovu wa adabu ni kiburi hauna maana wala thamani yoyote. @Apigiwapo mbwa huparudia @Aumiaye ndiye hufunga mlango @Gogo halianguki mara mbili @Kinywa kilacho kisisikike,hupiga yowe kisisikike. @Mwenye kovu usidhani kapowa @Waume wala,mafala walipa @Maji na yachemke vipi hayasahau kwao baridi @Anapopaogopa mwanaume husindikizwa. Swala la wiki; Eleza tofauti ya methali na vitendawili.

No comments:

Post a Comment