Thursday, October 28, 2010

SURA MPYA YA RWANDA

Mnamo tarehe ya 7/4/1994,nchini Rwanda kulitokea mauaji ya haraiki ambayo yameangamiza idadi ya watu miliyoni moja. Kuanzia hapo, jamii ya wanyarwanda iliyokuwa ikinawili myaka mingi imeangamizwa sana na hivyo vikasababisha surs mbaya mahali pote duniani kuwa RWANDA NI NCHI YA KUHOFIA,NCHI AMBAYO HAIKUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU NA MENGINE MENGI MABAYA. Leo nchi hiyi, baada ya mauaji ya 1994,inaelekea kuwa nyota ya Afurika. Utajiri wa nchi unazidi kupaa, kila mwaka kunarekodiwa asilimia nzuri ya kupanda kwa uchumi. Mwamko wa siasa nchin humo unalenga umoja wawanyarwanda bila ubaguzi wa aina yoyote. Elimu nayo haikuwekwa pembeni, ushhidi ni kuwa idadi ya wanafunzi kuanzia shule za msingi kufika vyuoni inazidi kupanda na hilo huenda likapunguza idadi ya wale ambao wamenyimwa haki zao za kujifunza kutokana na siasa mbaya zilizopatikana nchini zamani.Hali kadhalika,huduma za afya zinapatikana kwa urahisi na watu wengi wanafundishwa kuhusu uboreshaji wa maisha yao na kukuza utajiri nyumbani mwao. Apigiwapo mbwa huparudia,wanyarwanda wamejifunza mengi kupitia mauaji ya watutsi ya 1994,wao(wanyarwanda) wameamuru kuwa kosa hilo halitarudia hata kamwe, kinacho wakela nyoyo ni namna wanavyoweza kufanya vizuri ili maendeleo yazidi kuongezeka. Aumiaye ndiye hufunga mlango, mtu anapopatwa na matatizo asingoje tu wengine wamsaidie kutatua. kila mwaka ripoti mbalimbali za mashirika ya kutetea haki za binadamu huonyesha kuwa Rwanda ni miongoni mwa nchi zinazonyanyasa binadamu lakini wengi wao hawajui nchi hiyi imetoka wapi na inaelekea wapi? Ikumbukwe kwamba asiyethamini chake hakika amepotea. Rwanda ni miongoni mwa nchi zinazoheshimu na kuthamini haki za viumbe vya Mola.

No comments:

Post a Comment