Wednesday, September 22, 2010

Russia haitaipa Iran maroketi Chapa S-300


 Mosko:
Urusi imeachana na mpango wa kuipatia Iran maroketi ya kisasa ya ulinzi, chapa S-300, ikiashiria juu ya vikwazo vya kimataifa dhidi ya Tehran. Jenerali wa Kirusi. Nokolai Makarov, alisema upelekaji wa silaha hizo utakuwa unakwenda kinyume na vikwazo ilivyoekewa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa afisa wa Urusi wa cheo cha juu kuhakikisha kwamba biashara hiyo imekwama, biashara ambayo ilizitia wasiwasi Israel na Marekani. Maroketi ya chapa S-300 ni  mfumo wa ulinzi wa masafa marefu hewani unaoweza kuhamishwa hapa na pale. Unaweza kuyagundua , kuyafuatilia na kuyaharibu maroketi na ndege zinazoruka masafa ya chini.

No comments:

Post a Comment