ANTANANARIVO
Rais wa zamani wa Madagascar Marc Ravalomanana jana alihukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela na kazi ngumu , kuhusiana na mauaji yaliyofanyika Februari mwaka wa 2009. Hii ni hukumu ya tatu dhidi ya Ravalomanana tangu aondolewe madarakani. Wakili wa Ravalomanana alisema rais huyo ambaye anaishi uhamishoni Afrika Kusini, alihukumiwa kwa kuhusika na mauaji na kuwa mshiriki katika mauaji. Februari mwaka 2009 walinzi wa rais Ravalomanana waliwafyatulia risasi wafuasi wa Andry Rajoelina, rais wa sasa wa kisiwa hicho na kuwaua watu 30 na kuwajeruhi wengine 100. Akiwa nchini Afrika Kusini, Ravalomanana aliikejeli hukumu hiyo akiitaja kama ya kipuuzi.
No comments:
Post a Comment