Saturday, August 28, 2010

Merkel ataka Wajerumani watoa msaada kwa Pakistan.


BERLIN
 http://www.dw-world.de/dw/0,,11590,00.html
HABARI ZA DW
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametumia hotuba zake za kila wiki kuwataka Wajerumani wawasaidie wahanga wa mafuriko Pakistan. Merkel pia alipuuzilia mbali madai kuwa msaada utapotea kwa sababu ya rushwa, akisema asasi za kiraia zitasimimia shughuli ya kusambaza misaada kwa waathiriwa. Kansela huyo wa Ujerumani pia alisema msaada kutoka kwa mataifa ya Magharibi huenda ukaleta matatizo ya kiusalama. Wakati huo huo ndege ya kijeshi ya shirika  la NATO iliyokuwa imebeba tani 100 za misaada ikiwemo genereta za umeme na pampu za maji zilizotolewa na serikali ya Ujerumani, imewasili katika uwanja mmoja wa kijeshi mjini Islamabad. Ndege ingine iliyobeba misaada kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali itaondoka leo, hapa Ujerumani.

No comments:

Post a Comment