Thursday, August 19, 2010

Kwa upande wako utajiri ni nini?

Mara nyingi tunasikia kuwa nchi za ulaya na Amerika ni nchi zilizoendelea wakati nchi za Afurika na Asia zingali ziko nyuma je maana yake ni nini? Kwa upande mmoja nchi iliyoendelea ni nchi ambayo imeelimika yaani yenye ujuzi au utaalam wa aina mbalimbali labda umepata kusikia mtu akinena salaale mzungu ameendelea kweli na ukimuuliza kwa nini anasema vile atakwambia tazama mzungu katengeneza ndege inayosafili angani au kuunda meli au kumpasuwa mtu akaondoa pafu moja halafu akamshona tena bila shaka tutakubali kuwa mtu anayeweza kutenda vioja kama hivyo ni mtu aliendelea kwa upande mwinginf tunaposema nchi fulani imeendelea tuna maana ya kusema kuwa nchi ile ni tajili ni nchi yenye mali nyingi au pato kubwa yenye bidhaa za kila aina nchi ambayo wenyeji wake wanaishi kwa raha kwa kuwa chakula cha kutosha wanalala kwenye nyumba nzuli wanavaa vizuli wanaelimisha watoto wao hawasumbuliwi sana na maladhi wanakaa kwa starehe nk. hali ya namna hiyi ndiyo hali ya utajiri .

No comments:

Post a Comment