Tuesday, March 08, 2011

Ni myaka mia moja tangu kuanzishwa kwa siku ya wanamama na myaka 36 Rwanda kuweka saini kwenye makubaliano ya kulinda haki za wanawake. Siku hizi idadi kubwa ya wanawake inakubaliana na unyanyasaji wa haki za wanawake kwa wao huwamini kwamba mwamke ni kiumbe dogo mbele ya mwanamume.Mama moja ametangaza kwamba lazima mme apige mkewe ikiwa hakutimiza matakwa ya mmewe. Wengine husema kwamba wanawake hawawezi kufanya kazi kama wanaume na huwenda hilo likageuka mwanzo wa kunyimwa haki zao kama haki ya kupata kazi za offisini,nk. Lakini tujiulize ni kweli mwanamke anyanyaswe kiasi hicho kutokana na mentiki za watu? Hilo kweli sikubaliani nalo wana wake wana nguvu za kufanya kazi kama wanaume na kuna mtafiti aliyesema kwamba wanawake wakipewa haki zawo waweza kutumika bola kuliko wanaume. Tuchukuwe mfano katika bunge la Rwanda wanawake ndiwo waongozao bunge hilo, wengine wanaongoza mashirika mbali mbali na wanasemekana kumudu kazi zao vyema. Kweli naona kwamba wanawake nao wana uwezo kama wanaume. Enyi wanawake muache tabia ya kujipinga mtumie akili zenu na uwezo mnao ili mjionyeshe katika jamii nzima kwamba mna uwezo. Wanaume nawo lazima wajue kwamba kidole kimoja hakivunji chawa, wakisaidiana na wanawake wanaweza kufika mahali pakuvutia

No comments:

Post a Comment